Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, wa halmashauri hiyo, kuchukua tahadhari na hatua za kimkakati katika maeneo yote ili kujizui mlipuko wa gonjwa wa Kipindupindu.
Mkurugenzi Mahera ametoa tahadhari hiyo, kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu katika wilaya jirani ya Longido katika mkoa wa Arusha, ambayo kimsingi, inapakana na halmashauri ya Arusha kwa upande wa Magharibi.
Amefafanua kuwa, uamuzi wa kuchukua tahadhari umekuja kutokana na mwingiliano wa kijamii, kibiashara na ukaribu wa maeneo kati ya wananchi wa Longido na wananchi wa halmashauri ya Arusha.
Aidha Dkt. Mahera ametaja mikakati inayoendelea kufanyika ni pamoja na kuhimiza usafi kwenye makazi binafsi na maeneo ya umma, kuhimiza matumizi ya vyoo, kudhibiti uuzaji hovyo wa vyakula vilivyopikwa pamoja na kuainisha vituo maalumu vitakavyotengwa kwa watu watakaopata ugonjwa huo.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewakumbusha wananchi mambo muhimu ya kufanya ili kujihadhari na ugonjwa wa Kipindupindu kama ifuatavyo :-
i. Kunawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula, na mara baada ya kutoka chooni.
ii. Kula vyakula vya moto.
iii. Kuchemsha maji ya kunywa.
iv. Kuosha matunda kwa maji safi na salama.
v. Kuacha kununua vyakula vya kupikwa kwenye maeneo ya wazi.
vi. Kufanya usafi kwenye maeneo yanayowazunguka.
Dalili za ugonjwa wa Kipindupindu ni kuharisha na kutapika, uonapo dalili hizo wahi kwenye kituo cha kutolea huduma za afya.
.....!!!!! KINGA NI BORA KULIKO TIBA...!!!!
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.