Halmashauri ya wilaya ya Arusha wilayani Arumeru, imejiwekea mikakati imara, kufuatia agizo la Serikali kila kaya kuwa na choo bora kimachotumika, ifikapo tarehe 31 Disemba 2018 na kampeni ya 'Usichukulie poa, Nyumba ni Choo'.
Mikakati hiyo imewekwa, kufuatia kikao kazi kilichokutanisha wadau mbalimbali wa afya ikiwemo, madiwani, wenyeviti wa vijiji na watalamu kuanzia ngazi za kata, vijiji hadi halmashauri, kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, chenye lengo la kupata matokeo ya utafiti wa hali ya vyoo kulingana na mabadiliko ya tabia za afya utafiti uliofanywa na shirika la SNV.
Matokeo ya utafiti huo, yamesababisha halmashauri, kuwa na mbinu thabiti, zitakazowezesha kila kaya inakua na choo bora chenye miundombinu ya kunawia mikono, mara baada ya kutoka chooni, ikienda sambamba na agizo la Serikali la kila kaya kuwa na choo ifikapo tarehe 31.12.2018.
Akizungumza wakati wa kufunguzi wa kikao kazi hicho, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Arusha, Anastazia Tutuba, amewataka watendaji wa kata na vijiji, kuweka mikakati thabiti kwenye maeneno yao itakayowezesha kila Kaya inakuwa na choo kinachotumika.
Amewataka viongozi hao, kutumia sheria ndogo za vijiji kuwabana watu wasio na vyoo, pamoja na kufanya ufuatiliaji wa nyumba kwa nyumba na kaya kwa kaya kukagua, endapo kaya haina choo kuwataja kujenga, kuepuka kuingia matatani ifikapo tarehe ya mwisho iliyowekwa na Serikali kupitia kampeni ya usichukulie poa, nyumba ni choo.
"Wananchi wanapaswa kutambua Serikali iko makini na Kampeni ya Usichukulie ya usichukulie poa nyumba ni choo, hivyo pitieni kila kaya kuwahamasisha kujenga vyoo bora na kuvitumia, na kuwaeleza madhara ya kukosa choo ifikapo Disemba 31, 2018" amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Akitoa matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali la SNV, linalojishughulisha na Usafi binafsi na usafi wa mazingira, Mratibu wa Shirika hilo, Jackson Wandera, amesema kuwa licha ya kuwa idadi ya kaya zenye vyoo inaongezeka lakini tafiti zinaonesha bado kuna changamoto kwenye tabia binafsi ya mtu kutokunawa mikono, mara baada ya kutoka chooni pamoja unawaji mikono kwenye hatua tano muhimu.
Wandera amefafanua kuwa, bado watu hawanawi mikono kwa kufuata zile hatua tano, za unawaji mikono, kabla ya kula, baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa chakula, kabla ya kumnyonyesha mtoto na...
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu, choo kipo lakini hakitumiki huku sehemu nyingine, choo kipo kinatumika lakni watu hawanawi mikono mara baada ya kutoka chooni, na kuongeza kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kujijengea tabia ya usafi binafsi na si kwa sababu ya kukaguliwa na serikali.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.