• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Arusha DC yaendelea kupata neema ya magari

Posted on: November 23rd, 2018

Katika kuendelea kubuni miradi  ya kuingozea mapato na kuiwezesha halmashauri kuendesha shughuli zake bila mkwamo wa kipesa, hamalmashauri ya wilaya ya Arusha wilayani Arumeru, imekabidhiwa gari la kubebea mitambo na mizigo mizito, aina ya Foton Auman, gari lililonunuliwa na halmashauri hiyo kupitia kampuni ya uuzaji magari ya Simba Motors, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ofisi za makao maku ya halmashauri hiyo, eneo la Sekei.

Halmashauri hiyo imeendelea kupata neema ya magari kwa mwezi huu wa Novemba, 2018, ikiwa gari hilo ni la sita kupokelewa na Halmashauri hiyo, baada ya kupokea msaada mwingine  wa magari matano, mapema wiki mbili zilizopita kutoka kwa kikundi cha Friend of German cha nchini Ujerumani, licha ya kuwa gari hilo limenunuliwa na halmashauri hiyo.

Akizumgumza wakati akikabidhi kadi na funguo za gari hilo kwa uongozi wa halmashauri ya Arusha, Mkurugenzi wa Kampuni ya Simba Motors, Brigedia Generali mstaafu, Maiko Luhongo amesema kuwa gari hilo ni jipya na limeagizwa kutoka kiwandani moja kwa moja na kuutaka uongozi wa halmashauri kulitunza gari hilo kwa kuajiri,  dereva mwenye sifa nauzoefu wa kuendesha magari makubwa ,waminifu na mwenye nidhamu ya kazi.

Mwenyekiti wa halmashaui ya Arusha, mheshimiwa Noah Lembris, amewapongeza wataalamu wa halmashauri ya Arusha, waliowezesha kupatikana kwa gari hilo, wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt. Charles Mahera, kwa kuwa lengo la kununua gari ni pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa mapato ya halmashauri.

Mwenyekiti huyo, amewataka watumishi  wote wa halmashauri,  kushirikiana kwa pamoja kulitunza gari hilo ili liweze kufanyakazi kwa ufanisi na kuzalishak jambo ambalo ndilo lilikuwa kusudi kubwa la kumiliki gari hilo.

Naya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt. Wilson Mahera, amefafanua kuwa, gari hilo litakuwa likikodishwa pamoja na kufanya kazi ya kusafirisha mitambo ya halmashauri hiyo inayotumika kutengeneza barabara za ndani ya halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa kazi za jamii.

Ameongeza kuwa, gari hilo litatumika kama chanzo cha mapato ya ndani ya halmashauri yao na kuthibitisha kuwa upatikanaji wa  mapato hayo, utawezesha kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta ya elimu, afya, maji pamoja na miundombinu ya barabara.

Hata hivyo Dkt. Mahera amewataka wananchi pamoja na wadau wa ndani na nje ya  halmashauri hiyo, kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kukodi gari hilo kwa kufanyia shughuli mbalimbali ili waweze kuimarisha mapato ya halmashauri yake.

“Niwaombe wananchi na wadau mbalimbali mjitokeze kwa wingi kukodi gari hili,  kwaajili ya kuwasaidia kufanya shughuli zenu kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmeisaidia halmashauri yetu, kuongeza mapato ambayo yatasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa hali ya chini” alisema Dkt.Mahera.

Mradi huo wa gari ni moja kati ya miradi inayotekelezwa na halmashauri ya Arusha yenye lengo la kuongeza pato la halmashauri na hatimaye mapato hayo kutumika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa halmashauri hiyo pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kutaka kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mhe. Noah Lembris (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera,  wakikata utepe ishara ya kuzindua gari na SM 12581 mara baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Simba Motors iliyopata zabuni ya kuwauzia gari hilo.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, akionyesha kadi na funguza za gari namba SM 12581 mara baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Simba Motors iliyopata zabuni ya kuwauzia gari hilo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mhe. Noah Lembris, akiliwasha gari la halmashauri hiyo,  mara baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Simba Motors iliyopata zabuni ya kuwauzia gari hilo.

Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wakiwa kwenye hafla  ya kupokea gari la halmashauri ya Arusha.




Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA NAFASI ZA UDEREVA TAREHE 28/12/2018 December 19, 2018
  • Orodha ya majina ya walioitwa kwenye Usahili siku ya Ijumaa tarehe 20/04/2018. April 13, 2018
  • Matokeo ya usaili wa kuandika, nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji Arusha DC April 20, 2018
  • Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa- NIDA kata ya Kiranyi April 20, 2018
  • Tazama zote

Habari mpya

  • *YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI

    February 19, 2019
  • Waziri Lugola akumbusha Jeshi la Polisi Arusha DC matumizi sahihi ya sheria

    February 16, 2019
  • *YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LA KUWASILISHA TAARIFA ZA KATA ROBO YA PILI, OKTOBA MPAKA DISEMBA 2018*

    February 15, 2019
  • *YALIYOJIRI ZIARA YA KATIBU MWENEZI CCM TAIFA - ARUSHA DC

    February 14, 2019
  • Tazama zote

Video

JPM aagiza watalamu wa Ardhi kuanzia ngazi ya halmashauri kusimamiwa na Wizara
Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.