Na. Elinipa Lupembe.
Halmashari ya Arusha imeendelea kusherehekea ushindi wa kwanza uliopatikanaa kwenye kilele cha sherehe za Nanenane, kwa kuwakabidhi zawadi za pongezi Wakulima na Wafugaji waliofanikisha halmashauri hiyo kuibuka kidedea, kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Mifugo na Mazao kwa halmashauri za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, kwenye maonyesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini 2020
Akikabidhi zawadi hizo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za halmashauri hiyo, licha ya kuwapongeza washiriki hao, amethibitisha kuwa ushindi huo wa halmashauri umetokana na juhudi za wakulima na wafugaji hao.
Ameongeza kuwa, halmashauri inapata urahisi wa kutekeleza majukumu yake, pale ambapo wananchi wake wanaonesha juhudi za kuiunga mkono pamoja na kutumia vyema fursa na huduma zinazotolewa na halmashauri yao. "Tunajivunia kuwa nanyi wananchi wetu, sisi kama Halmashauri bila nyinyi wananchi, hususani wakulima na wafugaji, hatuwezi kutekeleza majukumu yetu wala mipango ya Serikali, lakini uwepo wenu na ushiriki wenu kwenye shughuli za serikali unaleta tija kwa maendeleo ya Taifa letu"amesema Mtambule.
Ameendelea kuwataka wakulima na wafugaji hao, kutumia fursa, utalamu na teknolojia za kisasa ili kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa kuzalisha mazao yenye ubora pamoja na kutumia mnyororo wa thamani katika uzalishaji huo, kwa kuongeza thamani mazao yanayoyazalisha.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtambule, amesema kuwa, licha ya wakulima na wafugaji kuanza kutumia teknolojia za kisasa na kufanya kilimo biashara lakini bado kuna changamoto ya utengenezaji wa bidhaa za mazao ya mifugo na kilimo zenye ubora pamoja na ushindani mkubwa wa masoko ya wazi.
Aidha ameweka wazi kuwa halmashauri ina mkakati wa kuanzisha eneo maalum kwa ajili ya wajasiriamali kuweka bidhaa zao, kwa lengo la kuwakutanisha pamoja awajasiriamali wa halmashauri hiyo, lengo likiwa kurahisha upatikanaji wajasiriamali hao, kuonyesha bidhaa na kupata masoko katika eneo moja.
"Halmashauri iko kwenye mazungumzo na wadau ambao wameonesha nia ya kuwekeza kweye eneo ambalo, litakuwa 'industrial area' ambapo wajasiriamali wa sekta zote watakaa hapo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao na eneo ambalo litakuwa ni soko la pamoja la kuonesha na na kuuza bidhaa hizo, hivyo niwatake wajasiriamali kuitumia fursa hiyo pindi itakapokuwa tayari"ameweka wazi Mkurugenzi huyo.
Jumla ya washiriki 6 walioshika nafasi tatu za mwanzo wamepatiwa fedha taslimu, ikiwa ni wafugaji watatu na wakulima watatu, na walishiriki wote wamepewa vyeti vya pongezi kwa ushiriki na kutakiwa kutolukata tamaa na kuendelea kujipanga kwa ajili ya maonesho ya mwaka ujao.
Hata hivyo wakulima hao, wameipongeza na kuishukuru halmashauri kwa kuwajali, kwa watalamu kuwafuata kwenye maeneo yao kwa kuwapa huduma za kitalamu, zinazowawezesha wakulima kufanya uzalishaji wenye tija na kupata mazao bora.
John Alfayo, ameomba kama halmashauri kuwa na maonesho ya wakulima na wafugaji yatakayo wakutanisha wote ili kufahamiana na kupata fursa ya kubadilishana uzoefu.
Maadhimisho ya nane nane hufanyika kila mwaka ambapo Kanda ya Kasikazini hufanyika kwenye viwanjwa vya Themi eneo la Njiro jijini Arusha.
PICHA ZA MATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.