Na. Elinipa Lupembe.
Katika kutekeleza mkakati wa Serikali ya awamu ya tano, wa kuboresha miundombinu ya shule na elimu kwa ujumla, halmashauri ya Arusha imeendelea kushirikiana na wananchi na wadau wa ndani na nje ya nchi, kuboresha miundombinu ya shule kwa kuongeza kasi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja ujenzi wa shule mpya za sekondari.
Akijibu swali lililoulizwa na diwani wa kata ya kimnyaki, mheshimiwa Olais Wavii, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa robo ya nne, aliyetaka kufahamu ni namna gani halmashauri imejikita katika kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, ilihali wananchi wamekuwa mstari wa mbele kutoa michango kwa hiari na kujenga vyumba vya madarasa, katika maeneo yao.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Dr Wilson Mahera, mesema serikali inatambua juhudi zinazofawanywa na wananchi katika kuhakikisha wananafunzi wanapata elimu kwenye mazingira rafiki, hivyo halmashauri inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo na kupata vifaa vya ujenzi, vitakavyowezesha kukamilisha ujenzi wa maboma hayo.
Aidha amefafanua kuwa kwa robo hiyo ya nne, wamepata jumla ya mifuko 180 ya saruji, ikiwa mifuko 100 imetolewa na Mbunge Viti maalum, mheshimiwa Amina mollel, mifuko 60 imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro, na mifuko 20 imetolewa na benki ya CRDB tawi la Sekei, na bado wanaendelea kutafuta wadau wengine kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu hiyo.
Hata hivyo Dkt. Mahera amezitaja baadhi ya shule za sekondari ambazo zimeonekana kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa, ikiwemo sokoni II, Kiranyi, Nduruma na Lengijave, na kueleza kuwa, tayari ujenzi wa vyumba vya madarasa umefanyika na kufikia baadhi yake kufikia hayua ya boma, na mkakati uliyopo ni kukamilisha maboma hayo, ili ifikapo Januari 2020, wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze shule bila kikwazo.
"Tutahakikisha hadi kufikia mwakani 2020 ujenzi wa vyumba vya madarasa vinakamilika kwa wakati, tayari kwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na madarasa ya Awali ."alisema mahera
Mkurugenzi huyo hakusita kuwapongeza wananchi wa halmashauri hiyo, kwa kuona umuhimu wa kuwa na shule za sekondari katika maeneo yao, kwa kuwapunguzia watoto wao adha ya kutembea umbali mrefu na kuamua kujenga shule katika maeneo yao.
Na kuthibitisha kuwa, jumla ya shule tatu mpya za sekondari zinatarajiwa kuanza mwaka ujao wa masomo, ambapo wananchi wa kijiji cha Likamba kata ya Musa, wanajenga shule ya sekondari Likamba, wanachi wa kata ya Oldonyowas, wanajenga shule ya Losinoni Juu na wananchi wa kijiji cha Kiserian wamejenga shule ya sekondari ya Kiserian kwa makubaliano na chuo kikuu cha Mzumbe, mchakato wa usajili wa shule hizo unaendelea kwa ajili ya kupokea wanafunzi mwezi Januari, 2020.
Ameongeza kuwa, ujenzi huo wa vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule za sekondari mpya na zile za zamani, unakwenda sambamba na umaliaziaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi pamoja na ujenzi wa mabweni na maktaba kwa baadhi ya shule.
Hata hivyo katika mkutano huo wa Baraza la madiwani, umefanyika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambapo, diwani wa kata ya Olturoto mheshimiwa Baraka Simon wa Chama Cha Mapinduzi, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na kuchukua nafasi ya diwani wa kata ya Oloirien mheshimiwa Albert Oltulele kwa tiketi ya CHADEMA. aliyeshika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Vyumba vya madarasa shule mpy ya Sekondari Likamba kata ya Musa, mradi unaotekelezwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Likamba na vitongoji vyake.
Nyumba ya walimu, shule mpya ya sekondari Likamba kata ya Musa,mradi unaotekelezwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Likamba na vitongoji vyake.
Vyumba vya madarasa shule ya sekondari Sikon II vinajengwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Japan nchini Tanzania
Vyumba vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi, mradi uliotekelezwa kwa nguvu za wananchi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.