Kitengo cha uchaguzi ni miongoni mwa vitengo sita vilivyopo chini ya Idara ya Utawala na Rasilimali Watu. Kinafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi. Kitengo cha uchaguzi kina Afisa mmoja (Afisa uchaguzi) anayehusika na shughuli zote zinazohusiana na uchaguzi.
Majukumu makuu za kitengo cha uchaguzi
•Kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unaendeshwa katika mazingira ya uhuru, haki na amani.
•Kuwezesha, kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na kupitia orodha ya wapiga kura walioandikishwa katika Daftari la Mpiga kura.
•Kuwezesha, kusimamia,na kuendesha uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, na uchaguzi wa serikali za mtaa.
•Kuhakikisha ngazi zote za uongozi zina wawakilishi kama kanuni zinavyotaka.
•Kupiti mipaka yote ya majimbo/maeneo ya uchaguzi nchini kwa lengo la uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa.
•Kuwezesha na kuhamasisha jamii juu ya masuala ya uchaguzi.
•Kusimamia na kufanya kutathmini mchakato wote wa uchaguzi katika maeneo ya uchaguzi..
MAFANIKIO
Kuratibu zoezi la uandikishaji wa wapiga kura ambapo Mwaka 2015, 79,603 (wanaume 42,382, wanawake 37,221) watu waliokidhi vigezo waliandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Kuwezesha na kuzimamia Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014; Wenyeviti 68, wenyeviti wa vitongoji 256, na wajumbe wa baraza la kijiji walichagulia.
Kuwezesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Mwaka 2015 ambapo madiwani 27 walichaguliwa, nafasi 9 wanawake viti maalumu waliteuliwa na mbunge 1 alichaguliwa.
Tathmini iliyofanyika baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuonesha mapungufu kwa baadhi ya nafasi za uongozi kutokana na viongozi waliochaguliwa kukosa na sifa za kuendelea kuwa viongozi kutokana na sababu mbalimbali kama vile kifo, kujiuzulu na/au kukuta rufaa. Hali hiyo ilipelekea kufanyika wa Uchanguzi wa Marudio kwa nafasi za Diwani mmoja Wenyeviti wa Vijiji 6, Wenyeviti wa Vitongoji 11 na nafasi 297 wajumbe wa Serikali ya Kijiji. Uchaguzi huo ulifanyika Januari,2017.Kitengo kinaendelea kuhakikisha kwamba nafasi zote za uongozi zinazobainika kuwa wazi zinapata wawakilishi wa wananchi kama sheria na kanuni zinavyoelekeza.
Pamoja na mafanikio yaliyopatikana Kitengo kinakabiliwa na changamoto kama vile:-
•Upungufu wa majengo ya kudumu ya serikali yanayoweza kutumika kama vituo vya kupigia kura nyakati za uchaguzi.
•Upungufu wa maafisa.
•Upungufu wa vitendea kazi.
•Kuwepo kwa mkanganyiko wa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Jiji.
•Kutokuwepo na uelewa kwa wanajamii kuhusiana na masuala ya uchaguzi na haki yao. Kwa mfano, wananchi wengi waliojitokeza katika kipindi cha kujiandikisha walitaka vitambulisho tu na siyo kwa ajili ya kupiga kura.
•Kujiuzulu kwa viongozi waliochaguiwa pasipo sababu.
•Wananchi kukiuka sheria na taratibu kwa kukusudia.
Kitengo kinaendelea kuratibu masuala ya uchaguzi kwa muongozo wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977 na sheria na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kuhakikisha kuna uhuru, haki na amani katika uchaguzi wa vyama vingi katika chaguzi zote.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.