Afya
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwa kutambua umuhimu wa Afya ya jamii chini ya mpango wa kuboresha afya ya msingi (MMAM) imeendelea kutekeleza majukumu yaliyo ainishwa katika sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007 .
Huduma za afya katika Wilaya ya Arusha hutolewa kwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wengine kwa maana ya watu na mashirika binafsi (Public Private Partnership) chini ya Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha zikisimamiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya.
Katika kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kama zilivyokusudiwa Idara ya afya imegawanyika katika vitengo vikuu 5 ambavyo vinavyofanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba huduma zinazotolewa katika vituo mbalimbali zinakidhi viwango vilivyowekwa.
Vitengo hivi ni kama ifuatavyo:
1. Uratibu wa Programu za Afya.
2. Uratibu wa Mipango.
3. Utawala na vitendea kazi.
4. Uratibu wa afya mazingira.
5. Uratibu wa Tiba.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.